Mwanamuziki na Muigizaji maarufu wa Marekani, Madonna (64) ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kuwepo kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa siku kadhaa.
Jumamosi iliyopita msanii huyo alikimbizwa hospitali baada ya kukutwa akiwa hajitambui.
Taarifa za kuugua kwake zilitolewa na Meneja wake wa muda mrefu Guy Oseary ambaye alithibitisha kuwa msanii huyo alipatwa na maambukizi makali ya bakteria.
Msanii huyo alikuwa katika hatua za mwisho za mazoezi kwa ajili ya tour yake ya miezi 7 ya dunia ambayo ilipangwa kuanzia Canada mwezi Julai na kuendelea katika miji 45 katika nchi mbalimbali.
Tour hii ambayo ni maalumu kwa kuadhimisha miaka 40 ya msanii huyo katika sekta ya muziki sasa imeahirishwa.
Mtaalamu mmoja wa afya ameeleza kuwa ugonjwa alioupata Madonna ulikuwa mbaya, ikiwa mgonjwa hapati matibabu sahihi na mapema huweza kupelekea viungo vyake kufeli na hata kifo.