Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madeleine achafukwa kisa Alikiba "Alinitaka"

Kiba Madeleine Madeleine na Alikiba.

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Madeleine maarufu kama The Tanzanian Lioness ambaye ni Video vixen, Mwanamitindo na pia msanii kutoka Tanzania, ameweka wazi kuwa alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Alikiba kuanzia Oktoba mwaka 2022 mpaka mwezi Februari mwaka huu.

Kwenye mahojiano na Wasafi FM amelalamika kuwa Alikiba alimnyanyasa kingono na kumtumia, kisha kumwacha bila kumtimizia ahadi ambazo alikuwa amemuhaidi awali kwenye mahusiano yao.

Kupitia Instastory pia mrembo huyo amepost video ambayo anaonekana akiwa kwenye gari la Alikiba wakienjoy pamoja na kupost baadhi ya chats zake na Alikiba.

"Alikiba ni mtu ambaye hawaheshimu wanawake, alinitafuta kwa ajili ya kazi ya video yake ila mambo yalikua tofauti alianza kunitaka," amesema mrembo huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live