Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madee naye atangaza kununua private jet

Madee Ndegeee Madee naye atangaza kununua private jet

Thu, 15 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva toka Manzese Music Baby (MMB), Madee amesema mwakani (2022) atanunua Ndege Binafsi (Private Jet), ikiwa ni moja ya ndoto zake.

Madee ametoa kauli hiyo wakati anamtakia Dogo Janja kheri ya kuzaliwa na kuwataka vijana kuzungumza ndoto zao kwa kuwa maneno yanaumba!.

"Mfano mimi mwakani nitamiliki private jet, nisipofanikiwa mniite Dog lakini dume, nipo pale nimekaa," amesema Madee.

Ikumbukwe baadhi ya Mastaa wa Afrika wenye ndege zao ni DJ Cuppy (Nigeria), Sulley Muntari (Ghana), Don Jazzy (Nigeria), Mikel Obi (Nigeria), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon).

Wengine ni Emmanuel Adebayor (Togo), P Square (Nigeria) Didier Drogba (Ivory Coast), Samuel Eto'o (Cameroon) na Cassper Nyovest (Afrika Kusini).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live