Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madee atajiwa Jimbo ambalo anatakiwa achukue

SENEDA 1 Madee atajiwa Jimbo ambalo anatakiwa achukue

Mon, 22 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Madee Seneda amesema, anapenda sana kuiangalia siasa na kuisoma, ila hawezi kuifanya japo huwa anatumiwa ujumbe na viongozi wa siasa kwamba, wampe nafasi ya uongozi kwenye Jimbo la Ubungo.

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Madee amesema siasa zina maneno mengi, ambayo unatakiwa uwe mjanja ili uweze kuwashinda watu ili ukitaka ugombee ndiyo upewe.

"Napenda kuingalia siasa na kuisoma ila siwezi kuifanya, kwa sababu ina maneno mengi ambayo unatakiwa uwe mjanja ili uweze kushinda, siasa ni maisha ila sijawahi kufikiria wala kuwaza, japo natumiwa sana ujumbe na maombi na viongozi wa vyama tofauti tofauti kwamba wanipe nafasi niongoze Ubungo au Udiwani Manzese, na wanatamani niingie kwenye siasa" ameeleza Madee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live