Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madee asema Tip Top kipaji siyo ishu, ataja cha muhimu (+Video)

215 24845610 1882753032040207 4037605309366140928 N TZW

Fri, 15 Dec 2017 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki Bongo, Madee amesema kabla ya kumtoa msanii mpya chini ya Tip Top Connection huchunguza kwanza tabia yake kuliko kipaji.

Gaza na Madee

Madee amesema wenye vipaji ndani ya Tip Top Connection ni wengi na hawezi kutoa wengi kwa wakati mmoja hivyo wanawachuja kwa kuangali mwenye tabia nzuri.

“Kila mmoja huwa tunampa muda wake wa kumchunguza kwanza kuanzia tabia na mambo mengine, sisi huwa hatuangalii sana vipaji, vipaji vipo vingi” amesema.

“Tukisema vipaji itabidi tutoke tukazoe watu wengi wanaojuaa kuimba, kurapa, sisi cha kwanza tunakaa na wewe tunaangalia tabia yako, tabia ndio ina mashiko sana kuliko vitu vingine” Madee ameiambia Bongo5.

Hivi karibuni Tip Top Connection wamemtoa msanii mpya, Gaza ambaye ametoa ngoma na Madee ‘Nanii’.

Chanzo: bongo5.com