Rais wa Manzese, Madee amemwaga Maua ya kutosha kwa Rapa Roma Mkatoliki kuwa hakuna rapa wa kumsogelea kwa sasa.
Madee ameeleza ni muda sana alikuwa anaficha uwezo wa Roma ila alikuwa anatambua kuwa anakitu kwenye ubongo wake.
“Kitambo sana nalifichia MAUA yake hili mtu lakini sikuzote nafahamu linakilakitu kwenye ubongo wake, IQ kubwa sana.. so ngoja tu leo nilipe maua yake maana huko lilipo mambo ni mengi linaweza kudanja muda wowote na mijegejo kule mjegejo buku jelo tu oya @roma_zimbabwe wee mnoma sana ukimtoa @maarifabigthinker hakuna Rapper anasogelea nyayo zako mzee wa Ngonjera unajua unajua unajua tena.” Aliandika Madee kupitia ukurasa wake wa instagram.