Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madee: Natamani mtoto wangu afate nyayo za Blue

Blue Son Madee: Natamani mtoto wangu afate nyayo za Blue

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Manzese na CEO wa MMB Madee anasema alimuomba Mr Blue apige picha hiyo na mtoto wake Mesut Dee kwa sababu akikua amuhadithie ukubwa na heshima ya staa huyo aliyepiga naye picha.

Madee amepost picha hiyo na kushusha ujumbe huu kwenda kwa mtoto wake akiwa na Mr Blue

"Nilimuomba Herry Sammir apige picha na mtoto wangu coz nina mengi nitakuja kumuhadithia pindi atakapoanza kujitambua na kutambua huyu aliepiga nae picha ni nani. Kifupi nitamwambia huyu ni mmoja wa mwanamziki ambaye hajawai kuishi maisha mengine nje ya ustaa"

"Robo tatu ya maisha yake ni ustaa na hiyo robo iliobakia alikua ananyonya kwa Mama yake. Anahitaji heshima ya hali ya juu kwenye mziki wa Bongofleva. So @mesut_dee amepata bahati kupiga picha na huyu mtu. Natamani makuzi yake yaje kuwa kama @mrbluebyser1988 mixer Bitoz mixer Muhuni"

Unatamani mtoto wako awe kama staa gani wa Bongo?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live