Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madee, Dogo Janja wanogesha Bundesliga

15833 PIC+JANJA TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

WASANII Madee Ali na Dogo Janja wamenogesha Ligi ya Bundesliga (Ujerumani) inayoonyeshwa na Startimes nchini.

Wasanii hao wameteuliwa kuwa mabalozi katika kuonyesha ligi hiyo ambayo kuanzia tarehe 14 itakuwa ikitangazwa kwa lugha ya Kiswahili.

Akizungumza na Mwanaspoti, Madee alisema kuwa kwake Balozi katika jambo hilo anaamini kutaongeza morali kwa watu kufatilia Ligi ya Ujerumani.

"Ligi ya Ujerumani ni miongoni mwa Ligi tano kubwa duniani kwahiyo hii ni fursa kwa Watanzania kuweza kuangalia Ligi hii tena wakiwa wanaisikia kwa Lugha ya kiswahili," alisema.

Wakati huohuo Meneja Masoko wa Startimes, David Malisa, alisema wametafuta wachambuzi makini ambao watakuwa wanatoa burudani kwa watazamaji wao huku lengo likiwa ni kuwa na kitu bora.

"Ikumbukwe Startimes pekee ndiotunaonyesha Ligi ya Bundesliga na sasa Burudani inaongezeka maradufu kwasababu mechi zitatangazwa kwa lugha yetu, lakini pia zitakuwa katika mfumo wa Hd," alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz