Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madebe Lidai amchana Diva: Kama hujazaa mpaka sasa ndiyo basi tena!

Madebe Divaaa Msikie Madebe alichosema kwa Diva

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji wa Filamu za Bongo, Madebe Lidai maarufu kama Nabii Mswahili amemchana mtangazaji wa Wasafi Media, Loveness Malinzi 'Diva the Bawse' kuwa iwapo mpaka sasa hajazaa itakuwa ngumu kuwalea watoto wake kwani umri wake tayari umeenda.

Madebe amesema hayo wakati akihojiwa na Diva na kudai kuwa siku hizi watu wanakufa mapema, hivyo ni vyema kuzaa ukiwa bado una nguvu ya kuwatunza watoto wako na kuwapa mahitaji yao ya msingi kabla hujaondoka duniani.

"Diva kama mpaka sasa huna mtoto hata mmoja umeshafeli, mimi naamini kuzaa ukifika miaka 30 ushafeli kuzaa, kwa sababu naamini mwisho wa kuishi sasa hivi ni miaka 45 baada ya hapo unaishi kwa bonansi ya Mungu.

"Kwa hiyo ukizaa una miaka 30 utamlea wewe mtoto mpaka utakufa lakini ukizaa mapema ukiwa na miaka 18 itafika hatua wewe utawategemea wale watoto vinginevyo unaweza ukazaa kizazi ambacho kitakuja kumiliki mali zako tu," amesema Madebe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live