Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Madadapoa kutoka Bongo wafurika Kenya kuwakamua wakulima

MAKAHABA Madadapoa kutoka Bongo wafurika Kenya kuwakamua wakulima

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama ulidhani madadapoa hufurika mikoa ya Kanda ya Ziwa pekee pindi wakulima wanapovuna na kuuza pamba, umekosea kwani hali kama hiyo pia imetokea katika eneo la Rift Valley nchini Kenya ambapo inadaiwa kuwa kaunti za Bomet, Kericho, Kisii, Nandi na Mlima Elgon zimefurika akina dada hao wakati wakulima wa chai wakianza kupokea bonsai ya malipo yao wiki hii.

Vidosho hao wanaotajwa kutoka nchini Tanzania, Uganda na Kenya kwenyewe wamedaiwa kuendelea kumiminika mjini Kericho tayari kutafuna jasho la wakulima hao.

Migahawa ambayo kwa muda haikuwa ikipokea wateja wengi, kwa sasa imefurika huku nauli za magari ya abiria katika barabara za kuelekea Kisii na Kericho zikiwa zimepandisha.

Kwa wakazi maeneo hayo wamesema hiyo ni hali ya kawaida ambapo wanakiri kuwa warembo kutoka nchi jirani za Tanzania na Uganda, vilevile, wamekuwa wakijumuika na wenzao wa Kenya kuvuna.

Kwa upande mwingine, wakazi wa eneo la Konoin, Kaunti ya Bomet wameeleza kukerwa  na hali hiyo kwa madai kuwa makahaba wanatumia mitego mingi kuwanasa na kuwaibia wanaume.

“Badala ya kukodisha vyumba vya malazi mbali na mji, wanapangisha karibu na ploti zetu ili kuwadhibiti wanaume kwa muda mrefu, kuhakikisha wanawakamua kila kitu,” anasema Ann Chebet muuzaji wa mananasi eneo la Ngoina Road.

Aidha, kituo cha kibiashara cha Mogosiek kimedai vyumba vya kulala vimejaa na kuwalazimu baadhi ya walevi kutumia vichaka.

“Makahaba wachanga na wale wenye umri mkubwa hufika hapa mapema na kukodisha vyumba ambapo huwapeleka wateja wao,” anasema Robert Kipkemoi mkazi wa Mogogosiek.

Isitoshe wamiliki wa baa na migahawa wameongeza mtaji kutokana na mazingira mazuri ya kufanyabishara na wanatarajia idadi kubwa ya wateja. Kipkemboi anasema ni jambo ambalo limekuwa likirudisha familia nyingi nyuma kimaisha.

Ikumbukwe kuwa Konoin ni eneo linalopatikana katika Kaunti ya Bomet ambapo idadi kubwa ya wakulima wa majani chai huwa wanatoka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live