Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Machungu aliyoyapitia Miss Tanzania Hoyce Temu

27231 Hoyce+pic TanzaniaWeb

Thu, 15 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Usiku mmoja katika Hoteli ya Slipway jijini Dar es Salaam haukupita hivi hivi, kuna jambo lilitokea.

Ingawa ni miaka 19 imepita tangu usiku huo tulivu, kuna jina la binti mmoja lilitengenezwa katika maisha yake.

Jumapili iliyopita, akiwa amejiinamia alikuwa akiifikiria safari hiyo, lakini kitendo cha kufiwa na binti yake lilikuwa ni jambo zito kwake kulibeba, inawezekana vipi.

Hoyce Temu si jina geni nchini, lakini historia ya maisha yake inaweza kuwa ilitengenezwa usiku fulani ya mwaka 1999 pale Slipway.

Ikiwa ni miaka mitano tu tangu mashindano ya Miss Tanzania yarejeshwe, Hoyce alitangazwa kuwa mshindi wa mashindano hayo na kuanzia hapo maisha yake yakawa tofauti.

Furaha yake haikuwa kuwashinda Ayan Hassan aliyekuwa mshindi wa pili wala Helen Ongara aliyekuwa mshindi wa tatu.

Furaha au huzuni ya Hoyce haikuwa kushiriki mashindano ya Miss World, kufukuzwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wala kutangazwa na rubani wa ndege ya British Airways kuwa Miss Tanzania huyo ni miongoni mwa abiria katika ndege hiyo.

Hoyce, ambaye baada ya kufukuzwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikwenda kusoma chuo kikuu Marekani sasa anasoma shahada ya Uzamivu (PhD) ya mawasiliano ya umma katika Chuo cha Mtakatifu Augutine (Saut).

Miaka 19 imepita, maisha ya Hoyce ni tofauti, sasa ni mama akiwa na kazi katika Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania kama Mtaalamu wa Mawasiliano wa Maendeleo.

Je kuna siku imewahi kumuumiza? Ndiyo. Amepita mambo mbalimbali, amepita misiba mbalimbali, lakini Jumapili iliyopita hawezi kuisahau kamwe.

Siku hiyo, Hoyce alipata msiba mzito kwa kufiwa na binti yake aliyekuwa na umri wa miezi miwili tu.

Binti huyo Chrystal Rania Sikutwa alifariki katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kutokana na matatizo ya moyo, ikiwa ni siku moja tu tangu warejee kutoka matibabu Afrika Kusini.

“Mtoto mzuri amekwenda, amekwenda kupumzika, napita kipindi kigumu, Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi,” anasema Hoyce kwa kifupi nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam.



Chanzo: mwananchi.co.tz