Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabinti ya Mwanafalsafa na Kama Unataka Demu (J-Moe) ipi ilikukosha?

Mwana Fa J Moe Mwanafalsafa na J-Moe.

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabinti (Mwanafalsafa) na Kama Unataka Demu (J-Moe) ni muingiliano wa mawazo ama kuigana?

Baada ya Mwanafalsafa na J-Moe kukutana katika kibao cha "Ingekuwa vipi" haukupita muda wakaja kukutana tena kwenye idea za nyimbo zao!!

Mwanafalsafa aliibuka na kibao alichokiita "Mabinti" huku Jmoe akija na "Kama unataka demu"

Wakati Mwanafalsafa alimshirikisha Miriam SK yeye Jmoe alimshirikisha Q chief pamoja na Solo Thang Ulamaa...

Mfanano wa nyimbo Wote waliegemea kwenye kusifia wanawake ambao walikuwa na majina na wasiokuwa na majina pia, Mwanafalsafa alionesha kuwa addi ted yaani dam dam wanawake wenye sifa tajwa... Huku upande mwingine Jmoe akihitaji demu mwenye sifa alizozianisha...

Watu maarufu waliotajwa na wote wawili 1. Mercy Galabawa Ila ataweza kuimba vipi Rnb kama Stara Hii ni sawa na Mercy Galabawa leo kuwa msela-Jmoe Mwili utakaokufanya upende love kama Mercy Galabawa Na macho yanayovuta kama ya Miriam wa Ikoa unaweza utangaze ndoa

2. Aminata Keita Kama nitataka mwanya nafahamu wapi nitapata Muite Aminata wa Keita.... Mwanafalsafa Tukisema Miss Aminata Keita haina noma IFM watakona muda wote ambao atasoma-Jmoe

3. Zay B, Jay dee & Ray C kifua kama cha Zay B, kiuno kama cha Ray C na pozi kama za Jaydee-Mwanafalsafa Nini Gado kama Zay B... Mrefu kama Basila... Designer Khadija mavazi akatuoneshee Kajala.. Nitaakikisha hakuna machozi kama Kama Jaydee Sitazuia akisema anakuja kama Sister p-Jmoe

4. Happiness Magesse Warefu warembo kama twiga mithili ya Happy Magesse Mrefu siyo mfupi na nyama siyo mwembamba Hewani kama Gesse kiuno kama Odemba-Solo Thang

5. Radhia wa Unique Sisters Miondoko kama faudhia Au ungependa kithethe mithili ya Radhia? - Mwanafalsafa Lafudhi iwe tamu siyo kithethe ka Radhia Hapo mimi nitadata kama Nature kwa Sonia-Solo Thang Wote wawili walitaja kusifia watoto wa matajiri Katika verse ya tatu Mwanafa anasema "Kuna mabinti wapo kamili kila idara Familia bora akili zisizolala"

Huku Jmoe katika verse ya kwanza akisema "Bora nitoke makumbusho niende zangu Knyama, kwenye watoto wa geti kali baba mama tajiri"

Pia wote waliwataja akina Seven, Kibibi na Regina NB: Huwa napata shida kuamini kama huu ulikuwa mgongano wa mawazo tu, japo wao walituaminisha hivyo!

Ila Kama unataka demu ya Jmoe ni my favorite! Je, wewe ipi ilikubamba, Mabinti au Kama unataka demu?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live