Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabeste: Ma-Director, Ma-Producer hakuna ubunifu

Mabeste Ds Mabeste: Ma-Director, Ma-Producer hakuna ubunifu

Mon, 19 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Mabeste amewachana wazalishaji na waongozaji wa muziki nchini kuwa wamekosa ubunifu katika kazi zao na kuifanya tasnia ya muziki nchini kuendelea kuporomoka kila kukicha huku ushindani nao ukishuka.

"Ma-Director hawatumii muda wao kubuni, wanaochiokifanya kwa asilimia kubwa ni kucopy na kupaste. Idea wanazichukua wanapojua wao ambazo zimeshafanyika mahali halafu wanaziweka kwenye hizi video wanazowafanyia Wabongo.

"Ni kama tu Ma-Producer anaweza akachukua wimbo wa msanii wa nje ya Tanzania akiamini huyu msanii hakuna anayemjua, Producer wengi wanafikiria kwenye hiyo angle hawatumii muda wao kubuni kitu ambacho atakuwa amekifanya yeye," amesema Mabeste.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live