Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabe.. Mabe.. Mabe.. Maberaa… (1949-2020)

Mabera+pic Mabe.. Mabe.. Mabe.. Maberaa… (1949-2020)

Wed, 30 Sep 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Kalunde Jamal KATIKA moja ya nyimbo kali za Bendi ya Msondo Ngoma kwenye miaka ya hivi karibuni ni Ajali. Huu ni utunzi wa marehemu TX Moshi William uliotamba mwaka 2016/2017 na mpaka sasa haujachuja. Achana na mistari mikali inayosisimua na ujumbe wa TX na sauti za kina Maalim Gurumo, Maina, Hussein Jumbe, Karama Regesu na Romario au mbwembwe za Ally Rashid.

Kuna mtaalam mmoja wa kupiga gitaa la solo. Ametembea kwenye solo humo ndani mwanzo mwisho na kudhihirisha utamu wake kina TX, Gurumo na wakongwe wengine wa Msondo wakati huo walishindwa kujizuia wakatumia sekunde kadhaa kutukuza jina na umahiri wake wakimba...”Mabe..mabe..mabee…maberaaa...” Huyu ni mkongwe Said Mabera, ambaye usiku wa kuamkia jana alifumba macho na kuamua kuagana na dunia hii. Aligoma kabisa kuliona tena gitaa na kutii amri ya Alah kwenda kuanza maisha yake mapya peponi. Dah! Pumzika Mabera, fundi ambaye gitaa lilikutii. Mashabiki wako walipenda kukuita Dokta kutokana na umahiri wako. Hata pamoja na Meneja wa bendi Said Kibiriti kuthibitisha safari yake ya mwisho bado mashabiki wake haswa wa Ilala na mitandaoni walikuwa hawaamini mpaka jana jioni walivyompumzisha kwenye nyumba yake ya milele.

Mabera alikuwa nguzo imara ya Msondo tangu enzi na enzi na ameshikiri katika nyimbo zote kali za Msondo hata akaendelea kuwa kisiki baada ya wakongwe kama kina TX, Gurumo, Suleiman Mbwembwe na wengine kutangulia mbele za haki. Sasa na yeye ameamua kuwafuata.

Amedumu kwa miaka 48 bila kuhama Msondo tangu alipojiunga nayo Juni mwaka 1973. Hakuamini kwenye kuhamahama zaidi aliheshimu ofisi yake iwe wakati wa shida ama raha.

Bendi hiyo awali iliyokuwa inamilikiwa na Chama cha Wafanyakazi imepitia majina mengi ikiwemo NUTA Jazz, JUWATA Jazz, OTTU Jazz na sasa Msondo Ngoma.

Haya ni mahojiano yake ya mwisho na Mwanaspoti mwaka 2013;

Chanzo: mwanaspoti.co.tz