Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maamuzi ya Mahakama yapelekea msanii ‘Kiss Daniel’ kutoka Nigeria kubadilisha jina lake

8323 Kiss Daniel 1 TZW

Thu, 24 May 2018 Chanzo: bongo5.com

/>

Kizz Daniel ambaye zamani alikuwa anaitwa Kiss Daniel

Kiss Daniel kuanzia jana Mei 22, 2018 alibadilisha jina lake na kujiita KIZZ DANIEL hii ni baada ya kumaliza mgogoro wake mahakamani na lebo iliyokuwa ikimsimamia mwanzoni ya G-Worldwide Entertainment .

Mwaka jana Kizz Daniel alikiuka masharti ya mkataba wake na G-World Ent. kwa kutangaza kufungua lebo yake ya Flyboy Inc, jambo ambalo lilipelekea uongozi wa G-World Entertainment kumfungulia mashtaka Kizz Daniel.

Mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu Mahakama mjini Lagos ilimpiga marufuku msanii huyo ku-perfom nyimbo zake zote alizotoa kipindi yupo chini ya lebo hiyo au kutumia jina lake kibiashara mpaka kesi itakapomalizika.

Kwa sasa Kizz Daniel tayari ameshabadilisha jina lake lililozoeleka la Kiss Daniel kwenye platform zote za muziki na kurasa zake za mitandao ya kijamii kama mahakama ilivyoamuru.

Chanzo: bongo5.com