Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Maajabu! Mrembo ajioa mwenyewe

Kshama Gupta Kshama Bindu

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Kshama Bindu raia wa India mwenye umri wa miaka 24 amekuwa gumzo mitandaoni baada ya kufunga ndoa ya kujioa yeye mwenyewe.

Harusi ya Bindu ilifanyika June 8 mwaka huu katika mfumo mpya wa harusi za tamaduni za watu wa India ambapo ameweka rekodiya kuwa mwanamke wa kwanza kufunga ndoa ya aina hiyo.

Bindu amesema alikuja na wazo la kujioa yeye mwenyewe ikiwa ni miezi mitatu imepita tangu alipoona mchezo kutoka Netflix unaofahamika kama Anne with AN E, mchezo uliomuonesha mtoto yatima ambaye alikumbwa na kadhia ya ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia tangu akiwa mdogo.

“Nataka kuwa muoaji na siyo mke.” Hatimaye mnamo Juni 8, akafanikiwa kujioa mwenyewe. Kshama Bindu amesema kwa kujioa mwenyewe anaweza kupata uhuru wa kuzuru sehemu yoyoteile aitakayo

Tangu kipindi hicho Bindu amepata wakati mgumu wakati akiwa anasafiri katika shughuli zake za kazini au katika manunuzi ya bidhaa magharibi mwa mji wa Gujarat ambapo amekuwa akiangaliwa kama mtu asiyekuwa wa kawaida na baadhi ya watu katika mji huo.

Aidha, Kshama Bindu amebainisha kuwa moja ya faida anayoipata ni kwamba atakuwa huru kuzuru sehemu yoyote ile aitakayo bila kuhitaji kibali cha mtu mwingine au kuwaza kuhusu mtu mwingine kuhamisha makazi kwa sababu yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live