Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maagizo ya halimu kesi ya Mwijaku na Nandy

MWIJAKU MAHAKAMANI Mwijaku na Nandy

Sat, 13 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi inayomkabili msanii wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga alimaarufu Nandy imeendelea katika mahakama ya mwanzo Sinza jijini Dar Es Salaam jana tarehe 12-8-2022.

Kesi hiyo ambayo imefunguliwa na Mtangazaji wa Clouds FM Burton Mwambe alimaarufu kama Mwijaku kwa madai kuwa alitumiwa vibaya na Nandy pasina makubaliano yake.

Mwijaku ameieleza mahakama kuwa, walielewana na Nandy afanye Tangazo kwa ajili ya Nandy Festival ambapo Tangazo hilo lilifanyika Hospitalini na baada ya Tangazo kukamilika Nandy alilikataa Tangazo hilo ila baada ya muda alikuta Nandy amelipost na wakashindwa kuelewa hivyo akaaumua kwenda mahakamani.

Kesi hiyo ilisikilizwa tarehe 9-8-2022 na ilipigwa tarehe mpaka jana tarehe 12-8-2022, baada ya Mwijaku kufika na Wakili wake pia Nandy kuwakilishwa na Meneja wake pamoja na wakili imepigwa tarehe tena mpaka tarehe 19-8-2022 hapo hapo mahakama ya Mwanzo.

Hakimu ameomba wahusika yaani mshitaki na mshitakiwa waje na nyaraka stahiki ikiwemo mkataba waliosaini kwa ajili ya tangazo hilo, endapo mmoja wao ataonekana ameenda kinyume na mkataba ule basi atamlipa mwenzake na madai ya Mwijaku ni kwamba anamdai Nandy Tsh milioni 10.

Baada ya kutoka mahakamani kwenye kesi yake na msanii wa Bongo Fleva @officialnandy @mwijaku amekataa kuzungunza kwa mara ya kwanza na media.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka tarehe 19 mwezi wa 8 mwaka huu 2022. Hakimu ametaka kuja na ushahidi ikiwemo mkataba wa Tangazo husika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live