Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maagizo ya Waziri Bashungwa kwenye Taasisi ya COSOTA

WhatsApp Image 2021 08 09 At 1.25.09 PM 2 660x400.jpeg Maagizo ya Waziri Bashungwa kwenye Taasisi ya COSOTA

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: millardayo.com

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ameaigiza Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kufanya kikao na Wadau ndani ya wiki moja na kuwapitisha katika marekebisho ya Kanuni ya Leseni ya Utangazaji na Maonesho kwa Umma ya Mwaka 2003.

Bashungwa ametoa agizo hilo Dar es Salaam alipofanya kikao na Menejimenti ya Taasisi hiyo kufuatilia marekebisho ya Kanuni hiyo ambayo imefanyiwa marekebisho ya tozo katika maeneo mbalimbali ya biashara yanayotumia kazi za Muziki.

.

‘’Ndani ya wiki moja kuanzia leo muende kwa Wadau mkawapitishe katika marekebisho haya ili nao watoe maoni yao, tulikamilishe hili kwa haraka ikumbwe kuna maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwa tunatakiwa kugawa mirabaha mwezi Disemba ni lazima mkamilishe hili kwa haraka”———Bashungwa



.

Bashungwa ameitaka COSOTA kuhakikisha inazingatia maoni yote ya Wadau ili kuepuka migogoro wakati kanuni hizo zitakapoanza kutumika.

Kwa upande wake Mwanasheria wa COSOTA Lupakisyo Mwambinga katika wasilisho lake la marekebisho hayo ya Kanuni hizo alifafanua kuwa baadhi ya maeneo yamefanyiwa marekebisho kutokana gharama za tozo zake kuwa na kiwango cha chini kisichoendana na gharama za maisha ya sasa sababu ni tozo za muda mrefu.



.



.

MESSI ASHINDWA JIZUIA AMWAGA MACHOZI MBELE YA WACHEZAJI WENZIE
Chanzo: millardayo.com