Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MUSIC FACTS: Shilole amnywea pombe Rayvanny!

Shilole Shishi Baby Shilole

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Ni msanii wa tatu wa Bongo Fleva kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram akiwa nao milioni 9.5, ametanguliwa na Diamond Platnumz na Hamisa Mobetto ambao ni wazazi wa Dylan.

Ila Shilole ni msanii wa kwanza wa kike anayechukuliwa kama mfano bora upande wa ujasiriamali na ameshinda tuzo nyingi upande huo kuliko hata kwenye muziki. Music Facts inakujuza zaidi;

1. Jina la Shilole alipatiwa na Bibi yake, maana ya jina hilo ni Kioo kwa Kinyamwezi, hiyo ni kutokana alipokuwa mdogo wakati akilia bibi yake alikuwa akimpatia kioo na pindi analipojiangalia alinyamaza.

2. Filamu ya kwanza Shilole kucheza kabla ya kuingia kwenye muziki inaitwa ‘First Decision’ ambayo alishirikishwa na Ray Kigosi, pia Irene Uwoya alikuwepo.

3. Wakati Shilole anaanza muziki, Q Chief ndiye aliyempeleka studio kwa C9 na alilipa Sh300,000 kwa ajili ya kurekodi, hilo limefanya Shilole na Q Chief kuwa na ukaribu mkubwa hadi leo.

4. Wimbo wa Shilole, Say My Name umeandikiwa na Barnaba wakiwa Afrika Kusini, huku kwenye kiitiko ukichukua maneno kutoka moja ya lugha za nchi hiyo. Video yake ndio ya kwanza kwa Shilole kushika nafasi ya kwanza kwenye chati za Soundcity.

5.Video ya wimbo wa Shilole, Malele iliyotoka Juni 2015 ndio video ya kwanza kwake kushutiwa kwenye nchi tatu tofauti ambazo ni Tanzania, Uholanzi na Ubelgiji.

6. Hadi sasa Shilole ameshaanzisha lebo mbili ambazo ni Shilole Entertainment (2016) akamsaini Amaselly na Shishi Gang (2020) akamsaini Ronze, lakini lebo zote zimeshindwa kufua dafu kwenye muziki wa Bongo Fleva.

7. Shilole na aliyekuwa mume wake, Uchebe ambaye ametokea kwenye video ya wimbo, Mchaka Mchaka, kwa mara ya kwanza walikutana Zanzibar kwenye sherehe ya kuzaliwa ya msanii Linah.

8. Wimbo wa Jay Melody, Najiweka ulikuwa wa Shilole na alipanga kumshirikisha msanii huyo, lakini baadaye Jay Melody akaamua kuuchukua na kuufanya wake na ulipotoka ukafanya vizuri.

9. Ilimbidi Shilole anywe wiski kidogo ili aweze kuchangamka na kucheza vizuri ‘scenes’ ya mahaba katika video ya wimbo Rayvanny, Natafuta Kiki iliyotoka Agosti 2016 ikiwa ni video yake ya pili chini ya WCB Wasafi.

10. Mwimbaji Snura kabla ya kutoka kimuziki ndiye aliyempaka ‘makeup’ Shilole kwenye video ya wimbo wa 20 Percent, Tamaa Mbaya aliyotokea. Kwa sasa Shilole na Snura ni wasanii wanaofanya vizuri kwenye Bongo Fleva na wote walianzia upande filamu kisha muziki ambao ndio umewapatia umaarufu mkubwa.

Chanzo: Mwanaspoti