Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MOBETTO BIFU LIMEISHA NA KAJALA

Mobetto Pic Data MOBETTO BIFU LIMEISHA NA KAJALA

Sat, 1 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

FEBRUARI 14 mwaka huu, haitakaa isahaulike kwa mwanamitindo Hamisa Mobetto na msanii wa Bongomovie Kajala Masanja.

Wawili hawa ambao ni marafiki walijikuta wakiingia katika ugomvi wa kurushiana maneno na kuvimbiana kwenye mtandao ya kijamii baada ya kuonekana kwa video za Kajala ambaye ni mtoto wa Kajala akiwa na msanii Rayvanny ndani ya gari katika mkao wa mahaba mazito.

Video hizo ziliwekwa na Rayvanny mwenyewe kwenye ukurasa wake katika mtandao wa Instagram ambapo zilizua gumzo na kumuharibia siku Kajala ambaye alikuwa visiwani Zanzibar akila bata na aliyekuwa mpenzi wake, Harmonize.

Jambo hili lilisababisha kufikishana polisi ambapo Kajala alikuwa akimtuhumu Hamisa kuhusika na tukio hilo kwa kile alichoeleza kuwa siku hiyo ya tukio mwanamitido huyo alimtoa ‘out’ binti yake huyo wa kipekee kwa ajili ya kupata chakula cha mchana.

Upande wa Hamisa naye alisema hatakaa kimya kwani amechafuliwa jina lake ukizingatia ni balozi wa huduma na bidhaa mbalimbali pia anamiliki kampuni zake jambo litakalomuweka katika wakati mgumu na wateja anaofanya nao kazi.

Ishu ilipamba moto kwelikweli huko mitandaoni, upande mmoja ulimlaumu Hamisa kuwa hata hivyo Paula sio saizi yake ya kuongozana naye kwenye mitoko kama hiyo na kutumia ule usemi wa ‘Mwana kuli-find mwana kuli-get’.

Wengine nao walimshutumu Kajala kwa kile walichoeleza amemlea mtoto huyo vibaya na hasa anapomrusha mara kwa mara mitandaoni jambo lililochangia watu wasio na nia njema naye kumsogelea, basi ilimradi tu kila mtu akasema lake.

Walivyomalizana

Habari za uhakika kutoka ndani zinaeleza kwamba baada ya ishu hii kufika pabaya, pande mbili za watu wa karibu wa wasanii hao ilibidi kuwaweka kikao cha pamoja.

Kwa upande wa Rayvanny shoo nzima ilisimamiwa na Babu Tale huku upande wa Kajala, muongozaji filamu maarufu na mtu wa karibu wa Kajala, Leah Mwendamseke ‘Lamata’ alisimama kumtetea msanii huyo.

“Kiukweli kesi ilikuwa imefika pabaya sana na ukizingatia pande zote hizo zilizokuwa kwenye mikwaruzano pia zipo karibu katika upande wa familia.

“Jingine kubwa walilowaza vipi ikifika mahali miongoni mwao sheria ikachukua mkondo wake na kumfunga, nani atafaidika katika hilo, hivyo waliona wakae chini wayamalize,” kilisema chanzo hicho.

Mara baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo, ndio kila mmoja akaanza tena kum-follow mwenzake kwenye Instagram.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz