Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MEJAKUNTA AWEKA WAZI KUTOKA NA MALKIA KAREN

Kareeeen MEJAKUNTA AWEKA WAZI KUTOKA NA MALKIA KAREN

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Msanii wa singeli Mejakunta ameweka wazi kwamba kwa sasa wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii malkia Karen na hawana haja kuficha machoni mwa watu.

MejaKunta amesema mahusiano yao yalianza kabla ya kutoa kazi waliyofanya pamoja pia wamepata ushawishi kutoka kwa wasanii wa kundi la NavyKenzo ambao wanafanya kazi huku wapo kwenye mahusiano.

“Ni rasmi kabisa tupo kwenye mahusiano hata watu wanaona jinsi tunavyo-play ‘party’ yetu na hatufichi tunaweka wazi hadi mitandaoni, mahusiano yalikuwepo kabla ya kazi ila tumeamua kutoa kazi ya pamoja kwa sababu wote ni wasanii hata Navy Kenzo wanafanya hiyo, mwanzo hatukuweka wazi ila baadhi ya watu ndiyo walikuwa wanajua” amesema Meja Kunta.

Sambamba na hilo, wawili hao kwa sasa wanafanya vizuri kupitia wimbo wao waliofanya pamoja uitwao ‘Sina’ wenye mahadhi ya Singeli.

Chanzo: zanzibar24.co.tz