Mshereheshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias 'MC Pilipili' amefunguka kuwa watu maarufu hupitia usumbufu na kuishi maisha ya utumwa sana katika mitandao ya Kijamii.
Pilipili amesema hii ni kutokana na kuwapa zaidi nafasi mashabiki ambao huja kuyaongoza maisha yao binafsi, "hivyo wanaamua wewe uposti nini au usiposti kitu gani".
Aidha, Pilipili amesema hali hiyo imepelekea watu maarufu muda mwingine kuishi maisha ambayo sio ya uwezo wao (wana-fake) ilimradi tu wawafurahishe wafuasi wao.
Pia, ameweka bayana kuwa hata yeye mwenyewe MC Pilipili aliwahi ishi maisha ya kwenye video akaja gundua kuwa kila kitu hufanywa kwa nafasi yake na kuamua kuachana kabisa na aina ya maisha hayo ya mitandaoni.