Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MC Mboneke azungumzia ushauri wa Roma Mkatoliki

Mc Pic Data MC Mboneke azungumzia ushauri wa Roma Mkatoliki

Thu, 20 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Siku moja baada ya msanii wa Hiphop, Roma Mkatoliki kumshauri mchekeshaji MC Mboneke kusajili ubunifu wake , naye atoa neno lake. Mc Mboneke ambaye jina lake halisi ni Oscar Mwanyanje, ametoa  neno hilo leo Jumatano Mei 19,2021 alipotembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi na kuzungumza mambo mbalimbali ikiwemo alichomshauri Roma kuhusu kusajili ubunifu wake. Msanii amejikuta akipata umaarufu kupitia clip zake fupifupi anazorekodi akiwa anakimbia na kuzungumza maneno kama irudiwe nk. Hata hivyo jana kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii Roma alionekana kumkubali msanii huyo na kuandika kuwa’ Yule jamaa anayekimbia huku anaji-shoot video clip, ameleta content nzuri kwenye comedy. “Naona raia wengi sasa wake kwa waume wanapita na hiyo idea, kama yeye ndio mbunifu halali wa kile kitu ningetamani sana kimlipe na anufaike kimtindo hapahapa yaani akiwa wa moto hivihivi! Akizungumzia ushauri huo wa Roma, MC Mboneke amesema ni wazo zuri na tayari yeye na menejimenti yake wameanza kulifanyia kazi. Pia anmeongeza kuwa kwake msanii kama Roma kukubali kipaji chake imempa faraja kubwa na kuona kuwa ana jambo zaidi anatakiwa kulifanya ili kuendele kuburudisha watu na kuwaelimisha kupitia kipaji hicho. Cha uchekeshaji alichojaliwa na Mungu. “Mtu kama Roma kukiri kwamba anakubali kibaji change kiukweli imenishtua na kunipa moyo, nimwambie tu kaka yangu ushauri wake nimeupokea na ninaufanyia kazi na ninahadi sitawaangusha mlioamua kuniamini na kunipa sapoti,”amesema Mc Mboneke.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz