Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MC Kinata amchana T.I.D, “nitamzimisha bure”

TID NA MC KINATA MC Kinata amchana T.I.D, “nitamzimisha bure”

Mon, 5 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku chache baada ya mkongwe Khalid Mohamedi ‘T.I.D’ kuwachana wasanii wa Singeli, mmoja wa wasanii wanaofanya muziki huo, MC Kinata naye ameibuka na kumjibu.

T.I.D aliwachaana wasanii wa singeli hivi karibuni kwa kuwaambia kuwa hawezi kutumia Mic wanayotumia wasanii hao wa Singeli na baadaye akarekodi kipande cha video na kuwaambia MC Kinata na Dulla Makabila kama wamemaindi, wamfuate pamoja awadunde mangumi.

Akizungumza na Wasafi TV, MC Kinata amesema, T.I.D anamheshimu kama kaka lakini kuhusu suala la kuwadunda, alikosea kuwasema hivyo.

“Namheshimu kama braza lakini suala la kutupiga hapo alienda kombo. Wewe niangalie huu mwili wangu na wake si ntamzimisha bure,” alisema MC Kinata ambaye anatamba kufanya muziki wa Singeli huku akichanganya na maneno ya Kingereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live