Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MB Dog kumpeleka Diamond mahakamani

Mb Dog  WA0002 MB Dog na Diamond

Sat, 15 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Mkongwe wa Bongo Fleva, MB Dog amesema kuwa atampeleka mahakamani superstar wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz pamoja na kampuni ya Ziiki Media kwa kile alichoeleza kuwa ni kutumia haki ya wimbo wake.

Akihojiwa na Clouds Media, MB Dog amesema;

"Google wimbo huu wa Mapenzi Kitu gani au ingia YouTube halafu ataona. Nenda kwenye more Information utaona jina la Msanii aliyeimba wimbo huu imeandikwa jina la Diamond Platnumz. Ubunifu kama huo lakini nikitaka kuutumia napigwa stop. Unapotaka kuutumia kwa ajili ya maisha ya familia ili nipate kitu chochote siwezi.

"Na wakati natunga huu wimbo mwaka 2008. Diamond alikuwa bado Sana kwenye Muziki. Nina ushahidi wote kuhusu huu wimbo tangu sikubya kwanza naandika mashairi. Producer alikuwa Man Water. Nilijaribu kuzungumza na management yake lakini nilikosa nafasi. Nilikwenda COSOTA namshukuru Madam Doreen alipambana kwa nafasi yake. Walifuatilia mwaka mzima bila mafanikio yoyote. Kuna kiongozi mmoja Serikalini aliniita nikajua nitapata haki yangu lakini nikaambia niachane na past niangalie future"

"Nikiusikia huu wimbo unalia huwa nakaa chini nafikiria hata maisha yangu ya kawaida na nyumbani ninavyopambana na familia yangu halafu Mimi siwezi kuiba, kukaba ambacho Mungu amenibariki ni kufanya kitu na kufanya watu waweze kupata burudani.

"Niseme ukweli Ngoma zangu kuanzia Latifa kwenye platform hizi sijawahi kupata pesa. Hakuna audio yangu yoyote ambayo sina leseni zote zimelipia ushuru. Wasanii wengi wa Bongo wanadhulumika lakini haki zao za msingi hawazipati," amesema MB Dog.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live