Uyoga unaweza kutumika kama mboga au supu kulingana na matakwa ya mtumiaji. Pia kama vilivyo vitoweo vingine, uyoga una aina mbalimbali za mapishi.
Leo katika makala haya tutaangalia jinsi ya kutayarisha rosti la uyoga.
Uyoga robo kilo
Siagi vijiko viwili vya chakula
Kitunguu maji kimoja kilichokatwakatwa
Pia Soma
- TANZIA: Kwa nini namlilia Sharifa Hussein Kalala
- KUTOKA LONDON: Neno ‘kuku wa kisasa’ linafundisha maana mbaya , kiafya
- USHAURI WA DAKTARI: Madhara yatokanayo na vinywaji hivi
Kitunguu saumu kilichotwangwa nusu kijiko cha chai.
Pilipili manga ya unga nusu kijiko cha chai
Mafuta ya kula vijiko viwili vya kupakulia chakula
Chumvi kiasi
Jibini kijiko kimoja cha kupakulia chakula
Jinsi ya kutayarisha
Osha uyoga vizuri hakikisha hauna mchanga hata kidogo kwa sababu huwa una tabia ya kutunza mchanga kama haukukaushwa katika mazingira mazuri.
Bandika jikoni sufuria unayotaka kupikia, ikipata moto weka siagi kisha ongeza uyoga na uukaange kwa dakika mbili ili ulainike.
Bandika sufuria nyingine weka siagi ikipata moto ongeza kitunguu maji ukikaange hadi kibadilike rangi kuwa kahawia kisha weka kitunguu saumu na uendelee kukaanga hadi viwe sawa.
Kisha weka nyanya na uache vichemke pamoja kwa dakika mbili, kisha mimina uyoga uliokwisha ukaanga, acha uchemke kwa dakika mbili, kisha ongeza pilipili manga na jibini na uiache iyeyuke na ukoroge.
Hapo rosti la uyoga litakuwa tayari kwa kuliwa na wali, ugali na vitu vingine kama apendavyo mlaji.