Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

M 2 The P amtaja mrithi wa Mangwea

PACHA M 2 The P amtaja mrithi wa Mangwea

Mon, 8 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rafiki wa karibu wa aliyekuwa mkali wa HipHop na freestyle Bongo Albert Mangwea, M 2 The P amewataja wasanii Country Boy na Jordan kama ndiyo wanafuata nyayo za Ngwea ambaye alifariki Mei 28,2013.

M 2 The P amesema hilo kupitia EATV & EA Radio Digital wakati akitoa mtazamo wake kuhusu miaka 7 kwenye muziki bila ya Albert Mangwea ambapo amesema "Kwanza namiss muziki wake, tarehe 28 tumetoka kuadhimisha miaka 7 bila uwepo wake, mimi nilikuwa Morogoro kwa mama yake na tumefanya misa zote za kumkumbuka makaburini na nyumbani, pia nina Tattoo ya sura ya Ngwea pamoja na maneno mazuri ya kumfariji"

"Napenda sana anachofanya Country Boy, nilikuwa natakaga kabisa nimrithishe kabisa awe kama "CowObama" kabisa anachofanya yeye ni uwezo wa kupita kama anavyopita Ngwea pia alikuwa anamfuatilia na kumsikiliza sana Ngwea kipindi yeye yupo mdogo"

M 2 The P ndiyo mtu wa mwisho aliyekuwa na marehemu Mangwea wakati wanarudi kutoka safari ya nchini Afrika Kusini kabla hajapatwa na umauti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live