Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lulu atamani mtoto

0a4ad12c7f4de5607b12daad90653682 Lulu atamani mtoto

Mon, 14 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MWIGIZAJI wa fi lamu nchini Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kuwa alitamani sana kuwa na mtoto alipofi kisha umri wa miaka 22.

Mrembo huyo alisema ingawa hadi sasa bado hajafanikiwa ila anaamini ukifika wakati wa Mwenyenzi Mungu atajaliwa kupata mtoto wake.

“Sikuwahi kuwaza kuolewa, ila nilitamani niwe na mtoto wangu nikiwa na miaka 22, nilitamani sana kuzaa, lakini mipango ya mwanadamu sio mipango ya Mungu, nina miaka 25 sasa na bado sijajaliwa mtoto, naamini wakati wa Bwana ukifika nitazaa,”alisema.

Lulu aliwahi kuvishwa pete ya uchumba na Francis Ciza maarufu kama Majizzo mwishoni mwa Septemba 2018 na mpaka sasa hakuna ndoa iliyofungika.

Chanzo: habarileo.co.tz