Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lulu alamba dili zito...!

Lulu Chawa.jpeg Lulu apiga dili zito...!

Fri, 13 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji Staa Elizabeth Michael (Lulu) ametangazwa kuwa Balozi wa Kampeni ya ‘Mvalishe Akasome’ inayolenga kusaidia Watoto wa kike wenye mazingira magumu kupata mahitaji ya Shule ikiwemo sare, daftari na vifaa vingine.

Lulu ametangazwa kuwa Balozi na Binti Salha Foundation mbele ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima Jijini Dar es salaam na kisha Lulu mwenyewe akapata heshima ya kuizindua rasmi kampeni hiyo.

Lulu amesema “Nitatumia umaarufu nafasi yangu, umaarufu wangu, mitandao yangu ya Kijamii kuendelea kuhamasisha kuhusu kampeni hii na kwa Wadau mbalimbali ambao watataka kuchangia hapo baadaye kutakuwa na maelekezo ya kuchangia”

Kabla ya kupewa rasmi Ubalozi, Lulu amekuwa akishirikiana na Binti Salha Foundation kama Mdau wa maendeleo ya Mtoto wa kike tangu mwaka 2019 ambapo kampeni iliwezesha Watoto 70 wa Chalinze, Dodoma na Iringa kupata sare za Shule na Mtoto mmoja kupata ufadhili wa masomo na hadi sasa yuko kidato cha tatu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live