Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lulu: Simfuatilii Majizzo

Lulu Majizo Lulu: Simfuatilii Majizzo

Wed, 21 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama unadhani staa wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu anatabia ya kumfuatilia mumewe kama ana mwanamke mwingine (michepuko) basi unajidanganya! Ametoa jibu kuhusu hilo na sababu juu.

Shabiki mmoja alimua kumuuliza swali hilo Lulu akichati na mashabiki wake kupitia insta story, kufuatia habari kubwa nchini Nigeria iliyogonga vichwa vya habari mwanzoni mwa wiki hii.

Habari hiyo ilihusu mume na mke, ambapo mke wa ndoa alifariki Dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari akimfuatilia kwa kumfukuzia mumewe ambae alikuwa kwenye gari lingine na mwanamke ambae imeripotiwa kuwa ni mchepuko wake.

Lulu ambaye ni mke wa Majizzo amesema; "Watu wangu wa karibu wananijua, mimi mwenyewe kuna muda sijifuatilii... Na kutofuatilia sio kwamba hujali. Ni kuchagua kuwa upande chanya ya kuepeusha matatizo yasiyo na suluhu.

"Yani ukifuatilia hakikisha utakacho kutana nacho unajua namna ya kutatua. La sivyo unakuwa umeongeza shida juu ya shida," amesema Lulu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live