Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lulu: Sijawahi Kupanda Bodaboda

LULU Hatari Lulu: Sijawahi Kupanda Bodaboda

Mon, 21 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ELIZABETH Michael au Lulu ni mwigizaji ambaye ni nembo ya Bongo Movies kwani alianza kuigiza akiwa na umri wa miaka mitano pekee!

Lulu amejikuta kwenye mabishano makali na baadhi ya wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii baada ya kudai kuwa, hajawahi kupanda usafi wa bodaboda hivyo ni mara yake ya kwanza.

Ishu hiyo imesababisha maneno mengi huku mwenyewe akiwashangaa kuwa mbona siyo ishu kubwa kiasi hicho? Lulu anasema kuwa, ni kweli ni mara yake ya kwanza kupanda bodaboda na amejikuta akiinjoi na kuupenda usafiri huo. Amesema; “Comment zimejaa jazba.

Sasa mnalazimisha nini? Sijawahi kweli. Bajaj sawa ndo ulikuwa usafiri wangu pendwa.Pikipiki kwa kweli nimepanda jana (wikiendi iliyopita) ila nimepentaa nitarudia…”

Hata hivyo, mmoja wa mashabiki wanaomjua vizuri Lulu alimtaka kuacha kudanganya watu na kujifanya ni tajiri wakati watu wanamjua alikotokea.

Shabiki huyo alidai si mara ya kwanza kwa Lulu kutumia bodaboda na kwamba huo ndiyo ulikuwa usafiri wake zamani.

Aliandika; “Elizabeth Michael umezaliwa na maisha ya kawaida sana unajifanya babkubwa kukejeli bodaboda umepanda sana nakujua toka ukiwa mtoto…”.

Kufuatia maelezo hayo, Lulu akaibuka na kumtaka shabiki huyo kushusha munkarihuku akisisitiza ni kweli hajawahi kupandabodaboda katika maisha yake yote yaliyopita.

Lulu anasema; “Punguza jazba kwanza, narudia tena sijawahi kupanda. Siyo kwenye maisha ya kawaida siyo sasa hivi. Niko Drip by Lizzy (duka lake la nguo Sinza, Dar) kama vipi njoo unipige…”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live