Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lulu: Nauza umbea wa Rubby na Majizzo

Lulu Majizzoges (29).jpeg Lulu: Nauza umbea wa Rubby na Majizzo

Sun, 17 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rubby kuibuka mtandaoni akidai kwamba Majizzo hataki kumsapoti kwasababu alimuomba rushwa ya ngono akanyimwa ndiyo maana amekuwa mzito kusapoti maswala ya Rubby.

Mashabiki wameenda kumvaa LULU ambaye ni Mke wa ndoa wa Majizzo wakimtaka aseme neno kuhusiana na tuhuma hizo nzito na za aibu alizotuhumiwa mumewe. Kama ilivyokawaida yake kwenye upande wa Majibu huwa hakwepeshi ameenda nao sambamba.

Akijibu komenti ya mmoja wa Mashabiki zake, Lulu amesema ni kweli ana ubuyu wa kutosha kuhusu sakata la mumewe na Rubby ila hawezi kuutoa kiholela kwasababu yeye ni mchaga anaichukulia kama fursa. Eliza amesema ukitaka akumwagie umbea wote nenda dukani kwake kanunue nguo mbili tatu kisha wewe utarudi na kapu la umbea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live