Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lulu: Mume wangu amenipenda nilivyo

Lulu Majizo Lulu na mumewe Majizo

Thu, 5 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lulu au Mama G; ni staa mkubwa wa Bongo Movies ambaye anasema kuwa, mtu yeyote anayefanya mambo ili kumharibia ndoa yake, ajue hatafanikiwa kwani mume wake anamfahamu vizuri na amemchunguza kabla hajamuoa.

Lulu anasema anasikitishwa na wanaomfuatilia maisha yake, wakati yeye hafuatilii maisha ya mtu yeyote.

“Mume wangu ananijua sana, hivyo maneno ya watu hayawezi kugombanisha ndoa yetu tunapendana na tushachunguzana sana.

“Anajua mengi mazuri na mabaya, ameniona na kunipenda nilivyo,” anasema Lulu ambaye ni mke wa ndoa wa Majizzo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live