Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lulu Michael atumia mstari wa Biblia kujibu kuhusu ndoa yake

70204 LULU+PIC

Wed, 7 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwigizaji Lulu Michael amefunguka kuhusu ndoa yake akiihusisha na mistari ya Biblia Takatifu kwa kusema kuwa ipo katika Mathayo 25:1-13.

Lulu ameeleza hayo leo Jumanne Agosti 6, 2019 kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram baada ya kuulizwa swali na mchungaji Mashimo aliyetaka kujua atafunga ndoa lini.

Mchungaji huyo alitaka kujua jambo hilo akijenga hoja kuwa tangu kutangazwa kwa ndoa ya msanii huyo mwaka unakaribia kuisha.

Lulu alivalishwa pete ya uchumba Septemba 30, 2018 na mfanyabiashara Francis Siza maarufu Majizo ambaye ni mmiliki wa EFM redio na TVE.

Akimjibu Mchungaji Mashimo kupitia ukurasa wake huo Lulu amesema, “Kaka yangu jibu la ndoa yangu linapatikana katika kitabu cha Mathayo 25:13 na useme Ameen.”

Kwa mujibu wa andiko hilo mstari wa 13 unasema ‘Basi kesheni kwa sababu hamuijui siku wala saa.”

Pia Soma

 

Chanzo: mwananchi.co.tz