Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lulu Diva aeleza undani wa ku-date na Rich Mavoko

Mon, 12 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki Bongo, Lulu Diva amefunguka ukaribu wake na Rich Mavoko na namna unavyokuwa ukiripotiwa.



Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Amezoea’ ameiambia Back Stage ya EA Radio kuwa hakuna mahusiano yoyote kati yake na Rich Mavoko na ni stori tu ambazo na wao wanazisikia.

“Rich Mavoko ni mshikaji wangu wa karibu sana na tunaongea mambo mengi sana, wala tulikuwa hatuzijali kwa sababu kila mmoja wetu anajua sio kweli au ni kweli katika moja,” amesema.

“Kila mmoja anajua ukweli ambao upo ndani ya moyo wake, tujawahi kuzizungumzia kwanza,” ameongeza.

November mwaka jana alipoulizwa kuhusu ku-date na Lulu Diva alisema wao ni marafiki wa kawaida tu.

Chanzo: bongo5.com