Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukamba asimulia alivyokwenda kwa mganga ‘alitaka kumtoa kafara mwanangu’

Lukambaaaaa Lukamba asimulia alivyokwenda kwa mganga ‘alitaka kumtoa kafara mwanangu’

Tue, 27 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mpiga picha maarufu Bongo, Lukamba amesimulia jinsi alivyowahi kwenda kwa mganga kufuatia kuwa na matatizo.

Alisema akiwa na wake wawili kuna mambo yalikuwa hayaendi sawa kuna dada alimshauri aende kwa mganga kujikinga asije kuwa anarogwa huku na huku, ndipo akaenda kwa mganga.

“Nilipofika akachukua kucha zangu na nywele, mara yakatokea mambo ya ajabu pale akaniambia inahitajika ng’ombe ya kafara. Nikaenda nyumbani lakini mambo yalikuwa magumu siku na hela.

“Nilihaha kweli ikabidi mpaka niende kwa baba yangu mzazi maana mganga aliniambia nisipotoa ng’ombe yeye hawezi kukubali kuua mtoto wake basi atamuua mwanangu,” alisema Lukamba.

Lukamba anasema baba yake naye alimnyima hiyo pesa ya kununua ng’ombe na mwishoni alimuambia asiwe na wasiwasi amuambie huyo mganga kama anataka kafara basi amuue yeye.

Hata hivyo, Lukamba alimaliza msala huo kwa kuswali na kumuomba msamaha Mungu kisha hakukutokea lolote mpaka leo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live