Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukamba amlipua vibaya H Baba ‘hana ukaribu wowote na Diamond’

Lukamba 1 Lukamba amlipua vibaya H Baba ‘hana ukaribu wowote na Diamond’

Fri, 23 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mpiga picha wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Lukamba amesema, msanii H Baba hana ukaribu wowote na Diamond bali anajaribu kujionesha tu yupo karibu naye.

Lukamba ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na moja ya televisheni ya mtandaoni akisimulia masuala mbalimbali yanayomhusu ndipo alipozungumzia ugomvi wake na H Baba ambao umeanza hivi karibuni.

“H Baba anazungumzia vitu ambavyo havielewi. Alikuwa kwenye gemu, akafukuzwa kule akaja huku na hasira zake ananizungumzia mimi eti ningetoka kwa wema, wema upi?

“Yeye hana sehemu labda anaongea na Diamond au anachati, hana ukaribu wowote, atoe screen shot kama anayo akiwasiliana na Diamond, ni futi mia anataka eti kujifanya lebo ya Wasafi anaijua anaijua wapi?” alisema Lukamba. Lukamba afunguka madai ya kumroga Diamond.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live