Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukamba alirogwa bila kujijua

Lukamba Mdskds Lukamba alirogwa bila kujijua

Mon, 14 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kurogwa si lazima uganga uhusike ila pia tabia njema ambazo mtu anaweza akazionyesha ingali si zake zinaweza kukufumba macho ukiamini ni mtu sahaihi kwako.

Kupitia Fresh Weekend ya #wasafifm hii juzi Novemba 12, 2022, aliyekuwa mpiga picha wa #Diamondplatnumz, @lukambaofficial ameweka wazi udanganyifu aliokuwa akitendewa na aliyekuwa mkewe, #Ceccy.

kwa mujibu wa Lukamba anadai Ceccy alibadilika kitabia ikiwemo kutoshtuka tena na hasira za mumewe pale hata anapokosea (Ceccy).

Lukamba anadai kuna majibu ya Ceccy yalimwaminisha kuwa mwanamke huyo tayari alikuwa amepata back up sehemu nyingine, hii ni baada ya Ceccy kumdanganya Lukamba kuwa yupo room anataka kulala wakati huo yupo Club huko DUBAI.

Licha ya Ceccy kujua mumewe kajua ukweli na kakasirika, bado mwanamke huyo hakuonyesha kushtuka zaidi ya kumuuliza mumewe ni nini Hukumu yake baada ya hapo, kitu ambacho si sahihi kwa watu waliooana.

Mbali na hayo yote, Lukamba amemuomba msamaha mkewe wa kwanza, #shuu akiamini ndiye mwanamke mwenye mapenzi ya kweli aliyempenda msela bila jina, baada ya kile Ceccy alicho kifanya.

Lukamba na Ceccy waliripotiwa kuachana mwezi mmoja uliopita ikiwa ni muda mfupi tangu Lukamba atangaze rasmi kuondoka WCB. Wengi wanaamini Ceccy alifuata Fame ya WCB na sio Mapenzi kwa Lukamba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live