Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukamba: Kujitoa WCB sio vita, Rayvanny sio mtoto

Lukamba Diamond Rayvanny Lukamba na Diamond

Mon, 15 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa fotografa maalum wa CEO wa WCB, Diamond Platnumz, Ashraf Lukamba amesema kuwa ANA mawasiliano mazuri na msanii Rayvanny na kuwaambia watu waache kuchukulia ugomvi iwapo mtu akihama kutoka ofisi moja kwenda nyingine.

“Niko vizuri sana na Rayvanny, mimi sio mtu ambaye nina tabia za kugombana na watu, kama hatuwezani nakaa pembeni nafanya mambo yangu, huo ni ushamba wa kugombana na mtu.

“Kwa nini mtu akitoka anakuwa msaliti? Hapana huo sio usaliti, mtu akiamua kutoka ameamua kuanza kufanya maisha yake, ameona anaweza kufanya mambo yake mwenyewe, sio mbaya.

“Kujitoa sio ugomvi, watu wasigombanishwe kwamba ukitoka sehemu basi inakuwa ni vita, sasa itakuwaje watu wasijitegemee? Hata wazazi wangetuchukia. Rayvanny sio mtoto mdogo, ameona waliotoka pale, anajua kuna kufeli na kufauli, ni yeye na kichwa chake,” amesema Lukamba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live