Aliyekuwa fotografa maalum wa CEO wa WCB, Diamond Platnumz, Ashraf Lukamba amesema kuwa hajawasiliana na msanii harmonize tangu alipoondoka kwenye Lebo ya WCB huku akidai kuwa huenda msanii huyo alikuwa na hasira zake.
“Sijawasiliana na Harmonize tangu aondoke Wasafi, mtu katoka na hasira zake katia block, sasa niwasiliane vipi? Kwa njia zipi? Mimi nifanyeje? Ikifika wakati wa kuwasiliana tutawasiliana.
“Alipoondoka aliona nimchape block huyu dogo, muziki ni ni vita. Alinichapa block kitambo sana, nadhani mimi ni mtu wa kwanza au wa pili baada ya kumpiga block bosi Sallam.
“Sijawahi kumwongelea Harmonize, kama alinihofia labda namsema nikiwa na Diamond mimi sina mazoea na Simba, sijawahi kumzoea kabisa Daimond. Ni mtu ambaye hatujazoea kabisa eti mpaka tukae tunamzungumzia mtu.
“Sina tabia ya uchawa ama roho mbaya kiasi hicho, ni mtazamo tu. Watu wengi hata wasanii wakikuona tu wanajua mamluki wa Diamond yuleee… utadhani umevaa sura ya Diamond usoni.
“Imekuwa tatizo kubwa sana mpaka kwa raia. Kuna mtu anakuchukia tu kwa sababu upo karibu na Diamond hadi media zinanikunjia kwa sababu nilikuwa karibu na Diamond,” amesema Lukamba.