Menu ›
Burudani
Mon, 13 Nov 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mwanamitindo na Influencer maarufu nchini Brazil, Luana Andrade (29), amefariki dunia baada ya kufanyiwa upasuaji wa 'Kupunguza mafuta kwenye maeneo tofauti' kwenye mwili wake, [Liposuction].
Jarida la People linaripoti kuwa, Upasuaji ulichukua saa mbili na dakika 30, Luana alipata mshtuko wa moyo na mishipa kuziba na kushindwa kupitisha damu.
Hospitali inasema sababu ya kifo ni Pulmonary Embolism, damu inaganda na kuathiri mzunguko wake kwenye mwili, mishipa ya damu na mapafu, ni tatizo linalo sababisha vifo vya wagonjwa wengi wanao fanyiwa 'Liposuction Surgery'.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live