Takriban miaka 27 imemgharimu rapa Lil Wayne tangu kuanza kwa safari yake ya muziki kufikia rekodi ya mauzo ya Diamond ambayo ameinasa leo hii kupitia wimbo wake wa “Lollipop” uliotoka mwaka 2008.
“Lollipop” ambayo lil Wayne alimshirikisha Static major ambae alifariki wiki mbili kabla ya kuachiwa kwa wimbo huo, unakua wimbo wa kwanza kwa Wayne kufikia mauzo hayo
Lollipo ndio wimbo wenye mafanikio zaidi katika maisha ya muziki ya Lil wayne ambapo ulitajwa kuifanya album yake ya “Tha Careter III” kuuza zaidi ya Units Million Moja katika wiki yake ya kwanza na kunyakua tuzo ya Grammy mwaka 2009 kama Best Rap Song.
Huuenda Rapa Lil wayne hivi karibuni akasheherekea tena kufikia mauzo hayo kupitia ngoma alizoshirikishwa kama “I’m The One” ya Dj khaled ambayo kwasasa imefikia mauzo ya Paltnum 9 (Units Million 9) na “Look At Me Now” ya Breezy ambayo imefika 8Platnum.