Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lokole: Ukiona picha nyingine ya Diamond,Harmonize wakiwa pamoja naacha kazi Wasafi FM

Harmonize, Diamond Wakutana Uso Kwa Uso Ikulu.jpeg Lokole: Ukiona picha nyingine ya Diamond,Harmonize wakiwa pamoja naacha kazi Wasafi FM

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumanne ya March 12, Diamond na Harmonize walirejea tena kwenye headlines baada ya kukutana, kula, kuzungumza na kucheka pamoja kwenye mwaliko wa Iftar ikulu ya Dar es Salaam. Jioni yake, picha na video zao wakicheka na kupeana mikono zikateka kurasa za Instagram na kuwapa uchizi mashabiki wao.

Wapo wanaamini kuwa wawili hao wameamua kufungua ukurasa mpya na kusahau yaliyopita. Lakini, wapo wengi pia wanaoziona furaha usoni mwa hitmakers hao kama maigizo tu, baada ya hapo maisha yataendelea kama kawaida.

Miongoni mwa watu wanaoamini kuwa Diamond na Harmonize kamwe hawatokuja kuwa na ukaribu tena kama zamani, ni mtangazaji wa Wasafi FM, Juma Lokole.

“Ukiona picha yoyote, picha yoyote unayoijua wewe baada ya ile Iftar kuisha, ukiona picha yoyote, mi naacha kazi Wasafi,” alisema Mtangazaji huyo Jumatano hii kwenye kipindi cha Mashamsham. “Hakuna mapatano, pale ni unafiki mkubwa umepita, walikuwa wanataka picha walikuwa wanataka kutrend dunia ijue.”

Msikilize zaidi Mtangazaji huyo hapo chini:

View this post on Instagram

A post shared by Wasafi FM (@wasafifm)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live