Mafanikio ya ngoma ya Jux, Enjoy aliyomshirikisha Diamond Platnumz hayawezi kuzungumziwa bila kumtaja Lody Music.
Akizungumza Jumatatu hii kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, muimbaji na mwandishi huyo wa nyimbo amesema alihusika katika kuandika wimbo huo.
“Mara ya kwanza S2kizzy alinicheck Jux tayari ameshapata chorus na bridge lakini Jux alikuwa anastruggle kwenye how ataanza verse,” amesema.
“Kwahiyo sasa S2kizzy tulikuwa na ukaribu sana na yeye kwahiyo nilivyoenda ndio nikaanzia ile ‘Leo acha tu leo ni niwaweke wazi’ nikamwandikia na kule kwenye ‘napenda nikilewa tupande juu ya meza’ kwahiyo nikaandika brother akaelewa,” ameeleza Lody na kuongeza kuwa Jux ndipo alipomuambia wafanye kazi.
Anasema hadi sasa ana kazi mbili na msanii huyo na kwamba amewaandikia wasanii wengine wakiwemo Nandy na Maua Sama.