Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Linex Sunday Mjeda amesema biashara ya kuwaandikia wasanii nyimbo aliikataa mapema na kuongeza kuwa wasanii wkati mwingine hukosa fadhila.
Linex kupitia kipindi cha Mgahawa cha Wasafi FM amesema kuwa moja yati ya watu aliyowahi kuwakataza wasiwaandikie wasanii nyimbo ni pamoja na msanii Marioo.
"Niliacha kuandikia watu kwa sababu watu hawana fadhila, unamuandikia wimbo mtu kila siku anafanya show, ukimomba hela anakwambia sina kitu.
"Unaona Kama #MARIOO, nilimkuta ameimba wimbo Studio flani, nikamwambi wimbo mkali akajibu wangu basi? Nimemuandika mtu kanipa kilaki na nusu''
"Nikamwambia hiyo utafanya milele na milele haitalipa, pambana na kipaji chako peleka muziki wako Wewe mwenyewe, #MARIOO alikuwa tayari ametoka lakini watu walikua wanamtumia zaidi kwenye kuwaandikia nyimbo," amesema Linex.
#TanzaniaWeb.Com