Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Linex Sunday atoa Dunia Nyingine

5bc56167c41816579c3e06d5b2ea6ea8 Linex Sunday atoa Dunia Nyingine

Sat, 29 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MWANAMUZIKI wa kizazi kipya, Linex Sunday, amesema tayari ameachia albamu yake fupi ‘EP’ ambayo inaitwa Dunia Nyingine ikiwa na nyimbo sita.

Akizungumzia albamu hiyo, alisema tayari ameshatoa baadhi ya nyimbo kutoka katika albamu hiyo ikiwemo Dunia Nyingine, huku akisubiri muda atoe nyimbo nyingine.

Alisema miongoni mwa wasanii ambao amewashirikisha katika kuikamilisha albamu hiyo ni Mimi Mirs mdogo wake na Vanesa Mdee pamoja na mwanamuziki Gemma.

“Ni mbivu au mbichi nisaidie kuwajuza na wale kwa kushiriki na marafiki zako nami nitashukuru,” alisema.

Linex alifanya vizuri na wimbo wa Salima, akiwa na mwanamuziki Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ lakini baadaye alipotea kabla ya kuamua kurudi tena kwa nguvu.

Chanzo: habarileo.co.tz