Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Linah sana amejipata

Linah 20943731 Linah sana amejipata

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamama kunako Bongo Flevani, Esterlina Sanga ‘Linah’ au ‘Ndege Mnana’ amesema, watu wengi wanamwambia kuwa anaonekana kama hana mtoto, lakini ukweli ni kwamba yeye ni mama wa kishua.

Linah ni mama wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Tracy aliyezaa na dairekta wa filamu za Kibongo, Shaban Mchomvu.

Mwimbaji huyo mwenye sauti matata, amesema kuwa, anaonekana mdogo au hana mtoto kutokana na namna anavyojiweka na kujitengeneza.

“Mimi ni mama wa kishua ndiyo maana wengine hawaamini kama nina mtoto kwa sababu ninajipenda na natamani mtoto wangu naye awe kama mimi,” amesema Linah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live