Menu ›
Burudani
Tue, 24 Oct 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mrembo kutoka kwenye anga la Bongo Fleva, Esterlina Sanga 'Linah' amesema amelazimika kumpeleka mwanaye akaishi na dada yake kuepuka marafiki zake wanaokuja kumtembelea nyumbani.
Linah amefunguka inshu hiyo alipokuwa akihojiwa Wasafi FM ambapo alisema, hataki mwanaye aone zile 'vibe' za marafiki zake wanapokuja kumtembelea.
"Sitaki kabisa aone haya mambo ya marafiki wanakuja nyumbani hivyo niliamua kumpeleka kwa dada yangu ndio anaishi huko.
"Huwa namfuata wakati wa likizo na nikimchukua huwa sina muda na marafiki zaidi ya kuwa naye yeye tu," alisema Linah.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live