Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Linah: Siogopi kumuomba mwanaume pesa

Linah 2 Linah

Sun, 15 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Esterlina Sanga au Linah; ni mwanamama mwenye sauti tamu kunako Bongo Flevani ambaye anasema kuwa, akiwa na mpenzi ni lazima amuombe pesa kwa sababu ni jukumu lake kumhudumia na haoni aibu hata tone.

Akichezesha taya na Ijumaa Showbiz, mrembo huyo mwenye mvuto wa aina yake anasema kuwa, mwanaume anawajibu wa kumhudumia mpenzi wake kwa kila kitu bila hata kuombwa.

“Kuna baadhi ya wanaume wanasema kuwa wao hawawezi kuwahonga wapenzi wao pesa, jamani kama ndiyo hivyo pisi kali zote watazisikia tu redioni, binafsi nikiwa na mpenzi wangu namuomba pesa ya kila kitu kwa sababu ni jukumu lake kunihudumia na sioni hata aibu kwa hilo,” anasema Linah; mama wa mtoto mmoja ambaye bado ngoma yake na Kayumba ya Umeniweza inagusa mioyo ya mashabiki wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live