Mwanamuziki Lilian Wassira amejitosa katika tasnia ya filamu baada ya kutamba katika muziki wa injili.
Hayo yamebainika wakati wa usaili wa wasanii chipukizi watakoshiriki kuigiza filamu uliofanyika katika Hoteli ya Green Light iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam.
Amesema filamu hiyo imetokana na albamu ya nyimbo yake ya injili inayoitwa Saa imetimia, itakayokuwa na nyimbo nane ambayo anatarajia kuizindua sambamba na filamu hiyo.
Alieleza sababu za kutengeneza filamu hiyo akisema: “Najua lugha ya picha inaongea zaidi kuliko ya maneno, hivyo nimeona wimbo huu niutengenezee pia filamu licha ya kuwa na video yake ili kufikisha ujumbe niliokusudia.”
Kwa upande wao, majaji waliokuwa katika usaili huo akiwemo Shamsa Ford wameahidi kuchagua wasanii wenyewe vipaji watakaoendana na filamu hiyo.
Pia alimpongeza Lilian katika kuibua vipaji vipya ambavyo mbele ya safari vitasaidia kuleta Ushindani katika solo la Filamu ambalo alidai lilianza kwenda mrama.